Mawakibu Husseiniyya katika mji wa Najafu zinaendelea na kazi ya kusaidia familia zenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Siku ya nne mfululizo mawakibu Husseiniyya zinaendelea kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipto kidogo katika mazingira haya magumu tunayo pitia kwa sasa ya marufuku ya kutembea, kupitia opresheni kubwa iliyo andaliwa ya kusaidia familia hizo.

Mawakibu za mkoa wa Najafu ni sawa na mawakibu za mikoa mingine, zimesimama imara na kutangaza kua zipo tayali kusaidia watu wenye mahitaji, hivi ndio alivyo eleza kiongozi wa idara ya mawakibu Husseiniyya bwana Abdu Muhammad, akaongeza kua: “Katika mazingira haya magumu ambayo taifa letu linapitia na ili kupunguza shida kwa wananchi wakati huu wa marufuku ya kutembea, mawakibu Husseiniyya zimesimama pamoja kusaidia familia za wahitaji, kwa kufuata maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kupitia opresheni ya kusaidiana kijamii”.

Akabainisha kua: “Tunagawa vyakula vinavyo kusanywa na watumishi wa mawakibu Huseiniyya kwa familia zinazo stahiki katika miji ya wilaya ya Hairah, familia hizo tumezigawa kwa maeneo na kila eneo limepangiwa muda wake, ili kuhakikisha tunafikia familia zote, sambamba na kuzingatia maelekezo ya kiafya katika uandaaji na ugawaji, kama sehemu ya kusaidia wananchi katika kipindi hiki kigumu cha marufuku ya kutembea”.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma zinaendesha mpango mkubwa wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, wameanza kutoa misaada hiyo tangu siku ya kwanza aliyotoa wito huo Marjaa Dini mkuu, hii ndio desturi ya mawakibu hizi wakati wa matatizo yanayo likumba taifa la Iraq, ambapo mara ya mwisho ilikua ni fitna ya magaidi wa Daesh zilipo simama imara kusaidia wapiganaji wa kujitolea na jeshi la serikali hadi wakapata ushindi na kukomboa ardhi yote ya Iraq”.

Kumbuka kua kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetangaza opresheni kubwa inayo fanywa na mawakibu zilizo chini yake katika mikoa tofauti ya Iraq, ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo katika wakati huu wa marufuku ya kutembea, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia familia hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: