Kuanza hatua ya nne katika mradi wa jengo la wagonjwa wa Korona

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha uangalizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, chini ya muda na ubora tarajiwa, wameanza hatua ya nne ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Korona, ambalo litakua ni sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala.

Hatua hii kwa mujibu wa maelezo ya Ammaar Swalaahu Mahdi katika mtandao wa Alkafeel: Itahusisha ujenzi wa vyumba (60) kwa kutumia vyuma, na itakua ni maandalizi ya hatu nyingine ya kufunga (Sandwiji panel) kwa kufuata vipimo vya kihandisi.

Akasisitiza kua: “Kazi inaendelea vizuri na inafanywa saa (24) kila siku”.

Kumbuka kua kazi hii ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu ya kuisaidia sekta ya afya, na chini ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kulinda jamii dhidi ya virusi vya Korona, mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Ataba tuufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi wameanza kujenga jengo maalum kwa ajili ya kuwatibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) ndani ya mkoa wa Karbala, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari ya Ataba tukufu na hospitali ya rufaa Alkafeel, ikiwa kama tahadhari kama ikitokea –Allah atuepushie- kupatika mtu atakae mbukizwa virusi hivyo katika mkoa huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: