Katika kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu mawakibu za kutoa misaada katika wilaya ya Balad, ambazo zipo chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimejiunga na opresheni kubwa ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa kufanya msafara wa kwenda kusaidia wahanga wa marufuku ya kutembea kwa sababu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Kiongozi wa ofisi bwana Hussein Ali Baldawi amesema kua: “Tumeanza kutuma misafara ya kutoa misaada kwa familia za mafakiri chini ya ratiba maalum, na tunatarajia kuzifikia familia nyingi zaidi, tumeanzia katikati ya mji hadi vijiji vya nje ya mji”.
Akaongeza kua: “Misafara yetu ilikwenda kwa awamu, kila awamu tumegawa vikapu (100) vya chakula mbalimbali, tukiwa na matumaini kua kitawasaidia japo kidogo kupunguza ugumu wa maisha katika familia hizo, msafara huu ni hatua ya tano, kazi ya kugawa chakula inafanywa usiku na mchana bila kupumzika, tunamuomba Mwenyezi Mungu ambariki kila aliye changia kupunguza shida za watu hususan wasamalia wema walio jitolea vitu hivi katika mazingira haya magumu”.
Familia za watu waliopewa misaada hii zimeshukuru sana namna Marjaa Dini mkuu anavyo wajali kama vile mzazi kwa wanae, sambamba na kutoa shukrani za dhati kwa waratibu wa misaada hii.
Tambua kua Marjaa Dini mkuu alitoa wito kwa mawakibu za kutoa misaada zilizo simama imara kusaidia wapiganaji dhidi ya magaidi wa Daesh, wajitokeze na kusimama vilevile katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, katika wakati huu mgumu wa marufuku ya kutembea kwa sababu ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, kutokana na wito huo Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.