Ndani ya wiki moja: Mawakibu za kutoa misaada katika mkoa wa Baabil zimegawa vikapu vya chakula (10,000)

Maoni katika picha
Ofisi ya Baabil chini ya idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kua, katika kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa sababu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona wamefanikiwa kugawa jumla ya vikapu (10,000) vya aina mbalimbali za chakula kupitia mradi wa Marjaiyyatu-Takaaful unao endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.

Haya ndio yaliyo semwa na kiongozi wa ofisi hiyo bwana Muslim Ni’mah Fatalawi, akaongeza kua: “Tangu ilipoanza opresheni ya kusaidia mafakiri na watu wenye kipato kidogo tumekuwa tukigawa misaada mbalimbali tunayo kusanya, na tumefanikiwa kuzifikia familia nyingi zenye mahitaji ya chakula, na kuzigawiya kapu zenye aina mbalimbali za vyakula”.

Akabainisha kua: “Mawakibu ya ofisi yetu imechukua jukumu la kugawa chakula katika mkoa wa Baabil, tumesha fanya utambuzi wa familia na tunagawa chakula kwa ratiba maalum usiku na mchana, japokua familia hizo ni nyingi kushinda uwezo wetu, lakini tunajitahidi kuwafikia wote, tutaendelea kugawa chakula hadi balaa hili litakapoisha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, tunaomba samahani kwa kila familia ambayo bado hatujaifikia, na tunawahakikishia kua tutawafikia na kuwasaidia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu”.

Familia za wanufaika zimemshukuru sana Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani pamoja na kamati iliyo ratibu misaada hii.

Tambua kua Marjaa Dini mkuu alitoa wito kwa mawakibu za kutoa misaada zilizo simama imara kusaidia wapiganaji dhidi ya magaidi wa Daesh, wajitokeze na kusimama vilevile katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, katika wakati huu mgumu wa marufuku ya kutembea kwa sababu ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, kutokana na wito huo Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: