Ofisi ya wanawake imefungua mtandao wa kuwasiliana na wanafunzi pamoja na wadau wake

Maoni katika picha
Idara ya ofisi ya wanawake chini ya Maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua mtandao wa kuwasiliana na wanafunzi wake pamoja na wadau wa maktaba na watafiti, kwa ajili ya kuwapa huduma wakiwa mbali kutokana na kushindwa kwao kuja maktaba kwa sababu ya marufuku ya kutembea iliyo wekwa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Huduma huu ni sehemu hatua zilizo chukuliwa na maktaba kwa ajili ya kuendeleza mawasiliano na wadau wake.

Wanawake wanaweza kuwasiliana kupitia ofisi ya wanawake kwa link ifuatayo (women-library@alkafeel.net) tunatarajia kupanua huduma siku za mbele kama hali itaendelea kua kama ilivyo –Allah atuepushie-.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na imeunda kamati maalum kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi hivyo, sambamba na kufuata maelekezo yote yanayo tolewa na idara ya afya, katika ngazi ya Ataba na majengo yake, ngazi ya mji mkongwe, ikiwa ni pamoja na kuzuwia mikusanyiko na kusimamisha swala za jamaa sambamba na kuahirisha baadhi ya harakati zake za kijamii na kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: