Mawakibu ya Khaaniqina inafanya opresheni kubwa ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Katika kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo onyesha ubinadamu wake kwa raia wa taifa hili, kiongozi wa mawakibu za Husseiniyya katika wilaya ya Khaaniqina bwana Haidari Juma Hussein ametangaza opresheni kubwa ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo, kutokana na mazingira magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa baada ya marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona.

Akaongeza kua: Hakika opresheni yetu ilianza tangu siku za kwanza yalipotolewa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, tumeweka mkakati wa kugawa vitu ambavyo vimekusanywa na wajumbe wa maukibu kwa ajili ya kuzipa familia za watu wenye kipato kidogo, misaada hiyo wameigawa kulingana na jografia ya wilaya, wamegawa vyakula vibichi na vilivyo pikwa, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuondolee balaa hili”.

Akasisitiza kua: Tutajitahidi kuzifikia familia zote na tutagawa zaidi ya mara moja kama tatizo likiendelea –Allah atuepushie-.

Kumbuka kua kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimetangaza opresheni kubwa kwa mawakibu zilizo chini yake, ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo wakati huu mgumu, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia familia hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: