Idara ya misaada tawi la Nainawa: Pamoja na majeraha yetu ambayo bado hayajapona hatuwasahau ndugu zetu mafakiri na tutasimama pamoja nao wakati wa shida

Maoni katika picha
Miongoni mwa idara za vijana zilizo ungana na idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya ni idara ya Nainawa, ambayo imejiunga na idara zingine katika kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo, wakati huu mgumu hapa Iraq kutokana na maradhi ya Korona, wameitikia wito wa Marjaa Dini mkuu na kujiunga na opresheni ya Marjaiyyatu-Takaaful inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara hiyo Shekh Nashwani Ismaili Shabki amesema kua: “Pamoja na majeraha yetu ambayo bado hayajapona tumejitolea kusaidia kwa kugawa vikapu vya chakula kwa famimia za watu wenye kipato kidogo ambao wapo katika eneo la mji wetu, tunatarajia kufikia idadi kubwa zaidi ya wahanga wa marufuku ya kutembea katika wakati huu mgumu”.

Akaongeza kua: “Kazi ya kugawa chakula tumeigawa kwa awamu, kila awamu tunagawa vikapu (100) vyenye aina mbalimbali za chakula”.

Familia ambazo tumezifikia zimeshukuru upendo mkubwa wanao onyeshwa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani aliye himiza mshikamano na kusaidiana katika kipindi hiki kigumu, pamoja na kuishukuru kamati iliyo ratibu misaada hii”.

Tambua kua Marjaa Dini mkuu alitoa wito kwa mawakibu za kutoa misaada zilizo simama imara kusaidia wapiganaji dhidi ya magaidi wa Daesh, wajitokeze na kusimama vilevile katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, wakati huu mgumu wa marufuku ya kutembea kwa sababu ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, kutokana na wito huo Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: