Muhimu… Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kamati ya habari na mawasiliano wanatoa huduma ya ziara kwa mbali

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweka utaratibu wa kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ukiwa mbali kwa watu ambao wapo ndani na nje ya Iraq, wameweka namba za simu za bure.

Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Farasi Abbasi Hamza ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Tumetengeneza mfumo wa kufanya ziara ukiwa mbali kwa kushirikiana na kamati ya habari na mawasiliano, mashirika ya simu (Zainu Asia na Kok) yamejitolea namba za kupiga simu bure na kufanya ziara kwa mbali ambapo zaairu atatuma ujumbe wa sauti”.

Akaongeza kua: “Mfumo huu unahatua nne kulingana na nguzo za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani pamoja na kuzunguka dirisha, kila hatua inavifaa vya mawasiliano”.

Kuhusu zana za ziara na namna ya kufanya akasema kua: “Ziara inafanywa kwa njia zifuatazo:

  • - Mtumiaji wa (Zainu Asia na Kok) apige namba (443) bure.
  • - Mtumiaji wa Kafeel apige namba (07602111000) bure.
  • - Ambaye yuko nje ya Iraq apige namba (009647602111000) lakini namba hiyo sio ya bure kwa sababu ni namba ya simu za kimataifa.
  • - Baada ya kupiga simu itajibiwa na ataambiwa uko chini ya Kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) omba haja zako hakika utajibiwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kisha utasikia mazingira ya haram na usome ziara.
  • - Wakati utakao pewa ni dakika moja, kisha simu itakatika moja kwa moja.
  • - Baada ya kupokelewa simu utahisi kanakwamba upo chini ya Kubba takatifu.
  • - Mfumo huu unaweza kupokea simu (1000) kwa saa mija na kuamiliana nazo vizuri bila shida yeyote.
  • - Huduma zote ni bure ispokua wale walio nje ya nchi tu”.

Kumbuka kua huduma hii imeanzishwa kutokana na tatizo la virusi vya Korona na maelekezo ya taifa ambayo Marjaa Dini mkuu amehimiza yaheshimiwe, serikali imepiga marufuku mikusanyiko ya watu kuhofia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaweka mfumo huu baada ya kukaribia ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, ambayo ni ziara muhimu sana katika mkoa wa Karbala, ili watu waweze kufanya ziara hiyo wakiwa mbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: