Kukamilisha usomaji wa ziara kwa niaba katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu kwa waumini wote wakiume na wakike

Maoni katika picha
Kikosi cha watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kilicho husisha masayyid na wanafunzi wa masomo ya Dini pamona na watumishi wengine wa Ataba, wamefanya ibada ya ziara katika haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa niaba ya waumini wote wa kike na wakiume kutoka kila kona ya dunia, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu Mahadi (a.f).

Wakati huohuo wamefanya ziara maalum kwa niaba ya madaktari na maaskari, wanao pambana kulinda taifa dhidi ya ukonjwa wa Korona.

Walinyanyua mikono na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Hashdi Shaábi na wa jeshi la serikali pamoja na wale waliokufa kwa maradhi ya Korona.

Kumbuka kua idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya ilitangaza kua inatoa huduma ya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa watu walio ndani na nje ya Iraq kwa kutumia namba maalum za kupiga simu bure.

Mfumo wa kufanya ziara kwa mbali umetengenezwa kwa ushirikiano wa kamati ya habari na mawasiliano, pamoja na makampuni ya simu ganja (Zain Asia na Kok) ambayo yalitengeneza namba za kupiga simu bure.

Mtumiaji wa mitandao hiyo anaweza kupiga simu bure kwa kutumia namba ifuatayo (443).

Huku mtumiaji wa mtandao wa Alkafeel Amniyya anaweza kupiga simu ya bure kwa kutumia namba ifuatayo (07602111000).

Walio nje ya Iraq wanaweza kupiga simu kwa kutumia namba (009647602111000) lakini namba hiyo sio ya bure kwa sababu ni simu ya kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: