Kuanza kwa mashindano ya hati bora ya mkono kwa lugha ya kiarabu ya Duaul-Faraji

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu Mahadi (a.f), idara ya mahusiana na vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya program ya kijana wa Alkafeel, inatangaza shindano la hati nzuri ya kuandika kwa mkono Duaul-Faraji (Allahumma kun liwaliyyikal-hujjatu bun Hassan, swalawaatuka alaihi wa alaa aabaaihi…) kwa lugha ya kiarabu.

Masharti ya kushiriki kwenye shindano hilo:

  • 1- Shindano litadumu kwa muda wa siku tatu.
  • 2- Yatatangazwa majina ya washindi watano siku ya Jumatatu sawa na tarehe (13/04/2020m) saa 11:00 alasiri.
  • 3- Andika majina matatu ya mshiriki, jina la mkoa, chuo au shule unayo soma, namba ya simu ya mshiriki, taarifa zitumwe kwa njia ya telegram maalum ya kijana mzalendo wa Alkafeel au kupitia me/alkafeel0
  • 4- Hati zitachujwa na (kituo cha nukta) katika maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Zawadi:

  • 1- Nakala za washindi wote zitachapishwa na kiwanda cha uchapishaji cha Atabatu Abbasiyya halafu watapewa.
  • 2- Mshindi wa kwanza na wa pili:

Watapewa pete ya fedha kila mmoja iliyo andikwa (Yaa Abulfadhil Abbasi) zilizo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na marashi kutoka katika haram takatifu.

  • 3- Mshindi wa tatu hadi wa watano kila mmoja atapewa pete ya fedha iliyo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya pamoja na tasbihi na marashi ya haram takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: