Kituo cha utamaduni wa familia kimeanzisha huduma ya kutoa ushauri kwa njia ya mtandao kwa wanawake tu

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeanzisha huduma ya kutoa ushauri kwa njia ya mtandao kwa wanawake, ili kutafuta utulivu wa nafsi katika familia, na kutatua changamoto za kijamii na kimalezi katika mazingira ya sasa.

Huduma hii ni sehemu ya harakati za Ataba tukufu katika kupambana na kuenea maambukizi ya virusi vya Korona, huduma hii inamfumo na ratiba kamili, imeanzishwa kwa ajili ya kuendeleza mawasiliano na wadau wetu hususan kipindi hiki ambacho tunahitaji mshikamano katika kila kitu, ikiwa ni pamoja na kwenye mambo ya kijamii, kimalezi na kiutamaduni.

Kituo kimesema kua unaweza kuwasiliana na mshauri wa kituo kila siku ispokua Ijumaa.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya ilianzisha kituo maalum kwa ajili ya mambo ya kifamilia, ili kusaidia malezi ya familia za raia wa Iraq na kutatua changamoto zinazo wazunguka, pia kinasaidia kupatikana utulifu wa nafsi katika familia, kimekua kikitoa ushauri wa kisaikolojia kwa wanafamilia na kufuatilia maendeleo yao chini ya watalam wa mambo ya familia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: