Maoni katika picha
Katibu mkuu huyo amefuatana na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, wameangalia maendeleo ya kazi na kusikiliza maelezo kutoka kwa watendaji pamoja na changamoto zao.
Katibu mkuu ameshukuru kazi nzuri inayo fanywa na mafundi hao kwaniaba ya Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya pamoja na watumishi wa Ataba, akasema kua: “Atabatu Abbasiyya inajenga kituo hiki kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, aliyehimiza kusaidia sekta ya afya pamoja na watu wanaosimama imara kuhudumia wagonjwa wa Korona, kila tatizo linalo tokea katika taifa letu Ataba tukufu husaidia kupambana nalo, ikiwa ni pamoja na tatizo hili la kiafya, haijajifunga kwenye kuhudumia mazuwaru peke yake bali inahudumia jamii yote, kituo hiki tunacho jenga katika mji wa Towareji kwenye hospitali kuu ya Hindiyya ni moja ya mchango wentu katika kuhudumia jamii, tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa maendeleo makubwa tunayo shuhudia, mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wamepiga hatua kubwa katika ujenzi wa kituo hiki”.
Kumbuka kua mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu walianza ujenzi wa kituo hiki siku ya mwezi (6 Shabani 1441h) sawa na tarehe (31 Machi 2020m), kama sehemu ya mchango wao katika kupambana na virusi vya Korona, kituo kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m1500) kitakua na vyumba vya wagonjwa 35 pamoja na chumba cha kutunzia vifaa vya usafi na chumba cha dawa.