Mkuu wa mkoa wa Karbala amesema: Sehemu yeyote ambayo serikali itahitaji msaada au jamii utaikuta Atabatu Abbasiyya ni ya kwanza kusaidia

Maoni katika picha
Mkuu wa mkoa wa Karbala Ustadh Naswibu Khatwabi amesema kua Atabatu Abbasiyya tukufu inamchango mkubwa sana katika kila sekta, kila sehemu ambayo taasisi za serikali zinahitaji kusaidiwa au jamii itaikuta Atabatu Abbasiyya ni ya kwanza kutoa msaada.

Akaongeza kua: “Ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala (Jengo la Alhayaat la pili), umefanywa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na kwa kuwasiliana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala”.

Akabainisha kua: “Mradi huu mkubwa umekamilika ndani ya muda mfupi tena kwa kiwango bora kiufundi na kiafya, ni dalili ya wazi kua raia wa Iraq wana akili kubwa na uwezo wa haji ya juu kama wakipewa fursa”.

Akafafanua kua: “Kituo hiki kitasaidia sana sekta ya afya na kitaendelea kua kimbilio kwa maradhi ya mlipuko hapa Karbala –Allah atuepushie-”.

Kumbuka kua kituo hiki kimetolewa zawadi na hospitali ya rufaa Alkafeel, watendaji wa mradi ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha ni sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya, pia ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na virusi vya korona chini ya muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, aliye amuru kujenga kutuo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: