Viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanakagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Hindiyya

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, siku ya Jumatatu asubuhi, mwezi (19 Shabani 1441h) sawa na tarehe (13 Aprili 2020m), ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Hindiyya iliyopo kusini mwa mkoa wa Karbala, mradi unao tekelezwa na mafundi wa kitengo cha uangalizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye uwanja wa hospitali ya Hindiyya.

Ziara hii ni kwa ajili ya kuangalia hatua iliyo fikiwa katika ujenzi wa mradi huo, ili kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya muda uliopangwa, kwa viwango vinavyo takiwa na wanufaika, makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu Mhandisi Abbasi Mussa ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kiwango cha mafanikio katika mradi huu kipo juu ya matarajio, kazi inaendelea vizuri, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mradi utakamilika na kukabidhiwa chini ya muda uliopangwa”.

Akaongeza: “Jengo limekalika kwa kiwango kikubwa, ikiwa ni pamoja na kufunga nyaya za umeme, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na juhudi za wajenzi tunatarakia kumaliza ujenzi baada ya siku saba kuanzia leo”.

Kumbuka kua mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu walianza ujenzi wa kituo hiki siku ya mwezi (6 Shabani 1441h) sawa na tarehe (31 Machi 2020m), kama sehemu ya mchango wao katika kupambana na virusi vya Korona, kituo kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m1500) kitakua na vyumba vya wagonjwa 35 pamoja na chumba cha kutunzia vifaa vya usafi na chumba cha dawa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: