Atabatu Abbasiyya tukufu umeunda (kikosi cha Hayatu-Twibi) kinacho husika na hatua ya baada ya maambukizi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Miongoni mwa shughuli zake za kupambana na virusi vya Korona, Atabatu Abbasiyya kupitia idara yake ya madaktari imeunda (kikosi cha Hayatu-Twibi) kinacho jumuisha vijana wa kujitolea walio pewa mafunzo ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona pamoja na nyumba za wagonywa hao.

Kiongozi wa idara hiyo Dokta Osama Abdulhassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika (kikosi cha Hayatu) kimepewa mafunzo ya kuamiliana na mazingira ya baada ya maambukizi, wamejikita katika mji mtukufu wa Karbala kama wasaidizi wakuu wa madaktari wanao pambana na virusi hivyo, wanafanya kazi saa (24) kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kua: “Kutokana na mafunzo waliyo pewa wanaweza kuingia sehemu zilizo ambukizwa, sambamba na kukagua sehemu aliyokua anaishi mgonjwa, pamoja na maeneo yanayo zunguka sehemu hiyo, halafu wanapuliza dawa na kutoa elimu kwa watu wa maeneo hayo”.

Akabainisha kua: “Kikosi hicho pia kinahudumia waliopona virusi hivyo, kwa kuwatembelea majumbani kwao na kupuliza dawa pamoja na kuendelea kuwapa elimu ya jinsi ya kuamiliana na wagonjwa wa Korona –Allah atuepushie-”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali katika kupambana na virusi vya Korona, pamoja na kufanyia kazi maelekezo yote yanayo tolewa na sekta ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: