Maahadi ya Quráni tukufu imepuliza dawa za kujikinga na virusi vya Korona katika nyumba zaidi ya (25000) mkoani Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya imepuliza dawa za kujikinga na virusi vya Korona katika nyumba zaidi ya (25000) mkoani Baabil.

Wamefanya kazi hiyo kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa na jeshi la wananchi.

Wamepuliza dawa vitongoji zaidi ya (25) vya mkoa wa Baabil, bado wanaendelea kupuliza dawa kwenye nyumba za makazi ya watu, misikiti na husseiniyya.

Kiongozi wa tawi la maahadi Sayyid Muntadhar Mashaikhi amesema kua: “Tunafuata maelekezo ya wizara ya afya ya Iraq katika kufanya kazi hii pamoja na muongozo wa Marjaa Dini mkuu na kamati ya afya”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali katika kupambana na virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kujenga vituo maalumu vya kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona, na kupuliza dawa katika vitongoji vingi vya Karbala sambamba na kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo kwenye mikoa tofauti, aidha imekua ikitoa elimu ya namna ya kujikinga na virusi hivyo kwa kutumia vipeperushi na vyombo vya habari ili kupunguza makali ya balaa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: