Kikosi cha Abbasi kimemaliza kupuliza dawa mitaa tisa ya makazi katika mkoa wa Diwaniyya kwenye eneo linalokadiriwa kufikia (2km16)

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapignaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kupitia kitengo cha kujikinga na Korona, kimepuliza dawa mitaa tisa katika mkoa wa Diwaniyya eneo linalokadiriwa kuwa (2km16), katika mkakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, kazi hiyo walianza kuifanya tangu siku za kwanza kupatikana virusi hivyo, wamesha puliza dawa kwenye miji mingi na mikoa tofauti, mkoa wa Diwaniyya ni moja ya sehemi ambazo wamepuliza dawa.

Bwana Ali Abdurahim mmoja wa wajumbe wa kamati ya kikosi cha Abbasi (a.s) inayo pambana na kuenea virusi vya Korona ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kamati ya kikosi cha Abbasi (a.s) pamoja na kamati ya kikosi cha opresheni ya Furat Ausat walianza kazi ya kupuliza dawa kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu alio toa kupitia Atabatu Husseiniyya tukufu, kamati hizo zimefanya kila wawezalo katika kuwahudumia watu wa Diwaniyya, tumepuliza dawa katika vitongoji na mitaa ya Jazaair, Dhwabaat, Taqiyya ya kwanza ya pili na ya tatu, na kwenye bustani za Hauli na mtaa wa Ramadhani, Mualimiin, Dauru Sakak, eneo lote jumla linakadiriwa kuwa (2km16) tumetumia zaidi ya lita (15,000)”.

Akabainisha kua “Jumla ya gari (30) zimeshiriki kwenye kazi hiyo”.

Akaongeza kua: “Kazi yetu haikuwa kupuliza dawa peke yake bali tumedoa huduma zingine za kibinaadamu, tumegawa vikapu vya chakula kwa familia kadhaa zenye uhitaji”.

Kumbuka kua harakati hizi zinatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata muongozo wa idara ya afya, pia ni sehemu ya mkakati maalum wa kupambana na kusambaa kwa virusi vya Korona hapa nchini.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi), kwa kushirikiana na shirika la Khairul-Juud wanaendesha opresheni ya (Hamlatu-Atwaa), ambapo walianza kupuliza dawa kwenye mitaa ya Karbala tangu tarehe (16 Machi 2020m), bado wanaendelea na kazi hiyo hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: