Kitengo cha sheria katika chuo kikuu cha Alkafeel kimetoa video ya kufafanua fatwa iliyotolewa na Marjaa Dini mkuu kuhusu kufunga mwezi wa Ramadhani wakati huu wa kusamba kwa maambukizi ya Korona

Maoni katika picha
Kitengo cha sheria katika chuo kikuu cha Alkafeel kimetoa video kuhusu fatwa iliyotolewa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani kuhusu kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati huu wa Korona.

Rais wa kitengo cha sheria katika chuo kikuu hicho Dokta Husam Ubaidi ametoa video inayo fafanua fatwa hiyo, amesema kuwa amefanya hivyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa watu wengi wanaotaka ufafanuzi wa fatwa iliyo tolewa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, kuhusu wajibu wa kufunga mwezi wa Ramadhani mwaka huu katika mazingira ya janga la Korona.

Video inamaelezo kamili pamoja na majibu ya maswali mengi ambayo watu wamekua wakijiuliza, pamoja na kulinganisha na misingi ya kifiqhi iliyo andikwa na wanachuoni kwenye vitabu vyao na risala amaliyya.

Ufafanuzi huo ni sehemu ya kuitumikia jamii kwa ujumla hususan wasomi wa sekula, na hilo ndio jambo kubwa ambalo linafanywa na chuo chetu.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu katika siku ya Jumamosi ya mwezi (17 Shabani 1441h) sawa na (11 Aprili 2020m) alijibu swali kuhusu kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani ya mwaka huu katika mazingira ya kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: