Kiwanda cha uchapaji Alkafeel: Kimetengeneza zaidi ya vifaa (10,000) vya kujikinga na maambukizi ya Korona

Maoni katika picha
Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji imechapisha zaidi ya vifaa (10,000) vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kila siku inatengeneza vifaa (1000) na kazi hiyo inaendelea hadi sasa, tumetengeneza ngome ya kwanza ya kitabibu kwa taasisi za afya za Karbala na Bagdad, tumesaidia kupunguza upungufu wa vifaa hivyo muhimu katika mazingira ya sasa.

Hayo yameelezwa na mkuu wa kitengo cha uzalishaji Mhandisi Raaidu Asadi, akaongeza kua: “Hakika vifaa hivyo vimesanifiwa na chuo kikuu cha Alkafeel na Karbala, jukumu la kutengeneza limebebwa na mafundi wanaofanya kazi katika Darul-Kafeel, nayo ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya katika mapambano ya Korona, sambamba na usaidizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia madaktari wake”.

Akasisitiza kua: “Vifaa hivyo vimeonyesha mafanikio makubwa sawa na vifaa vingine vya aina hiyo kitiba, kwani vimetokana na usanifu wa madaktari”.

Kumbuka kua juhudi hizi ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kuunganisha nguvu na kusaidia sekta ya afya, na muongozo uliotolewa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya wa ulazima wa kufanya tafiti za kielimu katika kipindi hiki, ndipo wataalamu na wabobezi wa chuo kikuu cha Alkafeel na Karbala wakaongeza juhudi ya kufanya tafiti mbalimbali za kugundua vitu vipya na kuboresha vilivyopo, kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, vifaa hivi vimetengenezwa kwa kutumia malighafi bora kiafya na kwa gharama nafuu tofauti na zilizopo sokoni kwa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: