Kiongozi wa Hindiyya na mkuu wa hospitali hiyo wamesifu kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kiongozi wa Hindiyya Mhandisi Muntadhiru Abdusataar Shaafi na mkuu wa hospitali hiyo Dokta Waathiqu Hasanawi, wamesifu juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu za kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hosptitali ya Hindiyya, kituo hicho kinajengwa kama sehemu ya kujiandaa kutoa huduma kwa wagonjwa wa Korona kama wakipatikana –Allah atuepushie-.

Mhandisi mkazi Karaar Barihi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kiongozi wa Hindiyya na mkuu wa hospitali ya hiyo wamekua wakitembelea na kuangalia ujenzi wa kituo hicho hatua baada ya hatua, ikiwa ni pamoja na ziara hii ambayo wamesifu kazi nzuri inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, jambo ambalo sio geni kwa Ataba, imekua ikitoa misaada ya kibinaadamu bila kusimama, hasa wakati wa majanga likiwemo janga hili la Korona”.

Kumbua kua ujenzi wa kituo hiki ni sehemu ya kusaidia juhudi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye kituo cha Alhayaat kilichopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa; wilaya ya Hindiyya ni miongoni mwa wilaya kubwa za mkoa wa Karbala na ipo umbali wa (km 20), mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala chini ya usimamizi wa kamati ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (mt 1500) kikiwa na vyumba (35) vya wagonjwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: