Kwa kutumia ufundishaji wa njia ya mtandao: Shule za Al-Ameed zinafanya semina ya kufundisha hati za kiarabu kwa watumishi wake

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed zinaendesha semina kwa njia ya mtandao ya kufundisha hati za kiarabu kwa watumishi wake, ili kuwajengea uwezo, semina hiyo inaenda sambamba na selebasi ya masomo kwa njia ya mtandao ambayo wakufunzi wanapaswa kujifunza.

Mkufunzi wa semina hiyo Ustadh Karaar Mussawi amesema kua: “Semina hii inalenga kuongeza uwezo wa walimu wa shule za Al-Ameed katika fani hiyo ambayo ni alama ya utamaduni wa kiarabu”.

Akaongeza kua: “Semina inahusisha jopo la wakufunzi na imejikita katika hati ya Raqaa, kuanzia namna ya kuandika herufi pamoja na namna ya kuziunganisha ili kupata neno, na kuunda sentesi kamili”.

Kumbuka kua Shule za Al-Ameed zinamkakati maalum wa kukuza elimu sambamba na kwendana na mazingira ya sasa, katika fani mbalimbali ndani ya mwaka mzima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: