Kiongozi wa idara ya afya ya mkoa wa Karbala amesema kua: Wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameonyesha kuwa wanaweza kufanya miradi mikubwa kwa muda mfupi

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya afya ya mkoa wa Karbala Dokta Swabahu Mussawi amesema kua wahandisi wa Atabatu Abbasiyya wameonyesha kuwa wanaweza kufanya miradi mikubwa ndani ya muda mfupi sawa na inavyo fanyika katika nchi zilizo endelea.

Ameyasema hayo akiwa na makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, siku ya Jumapili asubuhi, mwezi (25 Shabani 1441h) sawa na tarehe (19 Aprili 2020m) walipo tembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali kuu ya Hindiyya kusini mwa mkoa wa Karbala, kuangalia maendeleo ya kazi na kiwango cha ukamilifu.

Akabainisha kua: “Kituo hicho kinajengwa kwa ajili ya kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali kuu ya Hindiyya kama ikitokea maambukizi ya virusi vya Korona –Allah atuepushie-”.

Akaongeza kua: “Kituo hiki kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ndani ya wiki mbili zijazo kutokana na juhudi za watendaji wa mradi”.

Akasisitiza kua: “Mradi huu unatupa ujumbe wa aina mbili, kwanza kuwatoa wasiwasi wakazi wa Karbala juu ya kuwepo kituo maalum chenye kiwango cha juu na vigezo vinavyo takiwa kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ujembe wa pili ni uwezo wa wahandisi wa Atabatu Abbasiyya wa kufanya mradi wowote mkubwa ndani ya muda mfupi kama inavyo fanyika katika nchi zilizo endelea”.

Kumbuka kuwa sehemu kinapo jengwa kituo ni kwenye uwanja wa wazi uliokua umetengwa kwa shughuli zingine, kwa hiyo katika hatua ya kwanza umetumika uwanja wenye ukubwa wa (2m1500) chini ya mkakati na makubaliano yaliyo fikiwa na upande wa wanufaika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: