Jarida la (Turathi za Karbala) ni jarida la kwanza hapa Iraq kuelezea turathi za Karbala

Maoni katika picha
Tangu Atabatu Abbasiyya tukufu ilipo anza kufanya miradi ya kielimu na kitamaduni ililipa umuhimu mkubwa swala la turathi, ndipo kikaanzishwa kituo cha turathi za Karbala, miongoni mwa matunda ya kituo hicho ni kuanzishwa kwa jarida la (Turathi za Karbala) ambalo linaandika turathi za mji huo na utukufu wake, pamoja na kuhuisha hazina ya elimu, jarida hilo limesajiliwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu hapa Iraq, linategemewa kwa tafiti za kielimu, linachapishwa na kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimataifa limesajiliwa kwa namba (2312-5489 PRINT ISSN) na online (ONLINE ISSN 2410–3292)) 3297 ISO) na kwenye Darul-Kutub ya Iraq kwa namba (1992) ya mwaka 2014m.

Kwa mara ya kwanza jarida hilo limechapishwa mwaka (2014m), lio ni mara ya nne katika jarida la sita la mwaka 2019m, jarida hilo limejaa tafiti muhimu za turathi kwenye mambo tofauti, ya kiislamu, kilugha, kijamii na kihistoria, kutoka kwa watafiti na walimu bobezi kutoka vyuo mbalimbali, ni jarida pekee linalo andika tafiti za kielimu na kibinaadamu kuhusu mji mtukufu wa Karbala, kwani hilo ndio lengo la kuanzishwa kwake, ili kutoa picha halisi ya mji huu na kuutofautisha na miji mingine, sambamba na kuonyesha madhila na matatizo yaliyo ukumba mji huu katika zama tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: