Idara ya shule za wasichana Alkafeel imeandaa program ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya shule za wasichana Alkafeel chini ya maktaba ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, imeandaa program maalum kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia siku ya kwanza.

Program yenyewe ipo kama ifuatavyo:

  • - App ya (Haqibatu-Swaaimu), inafanya kazi kwenye simu ganja za kisasa (smart phone) ina ibada za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  • - Hatua ya pili ya shindano la (Misku-Nnajaat) kuna maswali ya Fiqhi, Aqida na masomo mengine.
  • - Ratiba ya (Qutufu Ramadhaniyya) itarushwa kwenye luninga ya Istighaathah.
  • - Shindano la (Rauhu wa Raihaani) kwa ajili ya mabinti wenye umri wa miaka (6) hadi (12) kuhusu kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s).

Program hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuongeza uwelewa wa Dini kwa mabinti, na kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuongeza maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: