Idara ya Quráni inajiandaa kutoa App maalum ya Quráni

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini kwa wanawake ambayo imefungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imekusudia kutoa App maalum ya Quráni katika harakati zake za mwezi wa Ramadhani mwaka huu wa 1441h.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kua: “Baada ya kufanikisha program ya (Khairu-Zaad) ambayo imekubalika sana, tumepata fikra ya kutengeneza App maalum ya Quráni, nayo itakua inasomwa Quráni kila siku na watu (150)”.

Akaongeza kua: “Lengo kuu ni kumuweka mtu karibu na Quráni kila siku, Mtume (s.a.w.w) anasema (Mimi nakuachieni vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, kama mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu)”.

Akasisitiza kuwa: “Kwakua kila siku tunashughulishwa na maisha muda wote, tumekaribia kuihama Quráni kama alivyo sema Mtume (s.a.w.w): (Ewe Mola hakika watu wangu wameihama Quráni), kwa kuzingatia hilo tumegawa visomo katika sehemu ya chini ya hizbu ili mtu yeyote asitoe sababu ya kukosa muda, hivyo mtu ataweza kufuatilia kisomo hicho bila kuathiri shughuli zake na hatapoteza thawabu katika mwezi huu mtukufu”.

Akabainisha kua: “Kisomo cha kila siku kitakua na hukumu za kifiqihi, elimu za malezi, elimu ya tafsiri, historia za Ahlulbait (a.s) pamoja na kumuunganisha mfuatiliaji na usomaji, ukizingatia kuwa harakati hiyo inatokea katika malalo ya mlindaji wa Quráni na kizazi kitakasifu Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Tambua kua idara ya maelekezo ya dini upande wa wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaharakati nyingi za kielimu na kitamaduni katika kipindi cha mwaka mzima, na kilele cha harakati hizo ni katika mwezi wa Ramadhani, Muharam na Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: