Watumishi wa kitengo cha kutunza haram wamemaliza kazi ya kupamba haram tukufu kufuatia kuingia mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kutunza haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kazi ya kupamba korido na milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kiongozi wa idara ya mapambo Ustadh Hasanaini Swadiq amesema kua: “Tumemaliza shughuli zote za upambaji wa haram tukufu, pamoja na kupamba jukwaa la kusomea Quráni katika mwezi huu wa Ramadhani”.

Akaongeza kua: “Tumeweka muonekano mpya kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani, mwaka huu unatofautiana na miaka iliyopita, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tumemaliza kazi zote”.

Tambua kua kitengo cha kutunza haram tukufu kina majukumu mengi yanayo husu haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kufagia, kupiga deki, kutandika miswala na zinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: