Maahadi ya turathi za mitume (a.s) kitengo cha wanawake inaendesha mashindano ya mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kitengo cha wanawake katika Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya siku ya Jumamosi mwezi (1 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (25 Aprili 2020m) kimeanza kufanya mashindano ya mwezi wa Ramadhani yaitwayo (mashindano ya Aashiqiin), yanayo onyeshwa kwenye toghuti na mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyo chini yake, kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona na marufuku ya kutembea.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa Maahadi hiyo Shekh Hussein Turabi: “Kutakuwa na mashindano ya aina nne ya kidini na kitamaduni kama ifuatavyo:

  • 1- Shindano la (kutoka kwenye Kitabu na Itrah) washiriki wa shindano hilo ni vijana wenye umri wa miaka nane hadi kumi na sita (wavulana na wasichana).
  • 2- Shindano la Maasumina 14 (a.s).
  • 3- Shindano la maswali kuhusu mwezi wa Ramadhani.
  • 4- Shindano la Sufratu-Ramadhaniyya.

Kutakuwa na zawadi zitakazo tolewa kila wiki kutoka kwenye malalo takatifu kwa washindi wa kila shindano, washindi watapatikana kwa njia ya kupiga kura”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: