Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ujenzi wa kituo cha Alhayaat ya tatu katika hospitali kuu ya Hindiyya

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha ujenzi wa kituo cha Alhayaat ya tatu, ambacho kimejengwa kwa muda wa siku (24) katika eneo la hospitali kuu ya Hindiyya, kama sehemu ya kusaidia taasisi za afya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Hiki ni kituo cha tatu kujengwa na Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha usimamizi wa kihandisi ndani ya mwezi mmoja, kituo cha kwanza kimejengwa katika mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, na kingine katika mkoa wa Najafu.

Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wamefanya kila wawezalo kukamilisha mradi huu ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora mkubwa, pamoja na changamoto za kiutendaji ukizingatia kuwa eneo kilipojengwa kituo hiki halikua limeandaliwa kwa jengo hilo, kwa kuwa walikuwa na niya ya dhati pamoja na moyo wa kazi wameweza kushinda changamoto zote na kukamilisha mradi, na umekuwa sehemu ya hospitali kuu ya Hindiyya”.

Akaongeza kuwa: jengo linaukubwa wa mita za mraba (1500) lina vyumba (36) kikiwemo chumba cha idara na dawa, kila chumba kinaukubwa wa (mt 3x5), kila chumba kina choo chenye ukubwa wa (mt 1.5x1.5) kina vitu vyote vinavyo hitajika, vigezo vya afya vimezingatiwa katika ujenzi huu, kazi zote zimefanywa chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya pamoja na idara ya afya ya wilaya ya Hindiyya na ile ya mkoa wa Karbala”.

Akasema kuwa: “Jengo linamfumo bora wa viyoyozi unao endana na mahitaji ya wanufaika, kuna mtambo maalum wa kuingiza hewa safi na kutoa hewa chafu, hali kadhalika kunamfumo wa viyoyozi unaofaa kuendelea kutumika hata baada ya tatizo la virusi vya Korona kuisha”.

Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo hiki umefanywa kwa ajili ya kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye kituo cha Alhayaat kilichopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa wilaya ya Hindiyya ni miongoni mwa wilaya kubwa katika mkoa wa Karbala na ipo kilometa (20), mradi huu umejengwa kwa ushirikiano na idara ya afya ya mkoa wa Karbala na kusimamiwa na idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya, utatolewa kama zawadi na hospitali ya rufaa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: