Kuanzishwa kwa program ya (Shadharaat-Usariyyah)

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanzisha program ya (Shadharaat-Usariyyah) chini ya kauli mbiu isemayo: (Familia yangu ndio amani yangu) kwa ajili ya kuchangia utulivu wa nafsi, roho na fikra kwa wanafamilia wote, pamoja na kuwasiliana nao katika mazingira haya.

Mkuu wa kituo hicho ustadhat Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “pamoja na changamoto za ugonjwa wa Korona, kituo hakijaacha kutoa msaada wa kinafsi, kijamii, kifikra na kifamilia katika kipindi hiki, kupitia jukwaa la mitandao kwa kutoa elimu na ushauri wa kifamilia, kazi ambayo walikuwa wanaifanya kwa kuwatembelea wahusika au wahusika kuja katika kituo”.

Akaongeza kuwa: Kutokana na kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani tumeanzisha program ya (Shadhiraat-Usariyyah), inayo husu kujibu maswali yote yanayo pokelewa na kitituo kutoka kwenye familia kupitia linki ifuatayo: https://forms.gle/joWUaHWt9dWgvkMa9
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: