Punguzo hilo ni sehemu ya kuonyesha mshikamano na wanafunzi wake kutokana na mazingira magumu ambao wananchi wanapitia kwa sasa, punguzo lipo kama ifuatavyo:
- 1- Ada ya masomo katika ngazi zote imepunguzwa mara ya pili kwa asilimia kumi (%10), katika mwaka wa masomo (2019/2020m).
- 2- Hivyo jumla ya punguzo katika mwaka wa masomo (2019/2020m) linakuwa asilimia ishirini (%20).
- 3- Mwanafunzi atanufaika na punguzo hilo (lililo tajwa kwenye namba moja) kwa kulipa ada kamili ya masomo kuanzia tarehe (29/04/2020m) hadi mwisho wa mda rasmi wa kazi katika siku ya Jumatano ya tarehe (20/05/2020m).
- 4- Punguzo la pili (lililo tajwa kwenye namba mbili) halihusishi wanafunzi waliopewa punguzo hapo awali kwa sababu maamum.
- 5- Wanafunzi watakao chelewa kulipa ada zao baada ya tarehe (20/05/2020m) hawatapewa punguzo lililotajwa kwenye namba moja.
- 6- Mwanafunzi aliyelipa pesa kamili katika muhula wa kwanza wa mwaka wa masomo ambao punguzo lake ni asilimia tano (%5) pesa hiyo itaongezwa kwenye muhula wa kwanza wa mwaka ujao wa masomo.
Kumbuka kuwa wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu imekipongeza chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kupunguza ada za masomo kwenye michepuo yake, kwani kufanya hivyo ni kuwasaidia wazazi wa wanafunzi, hayo yamo katika barua ya kukipongeza chuo hicho kutoka wizarani.