Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imeandaa ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia ofisi ya masomo mtandao, imeandaa ratiba maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mwaka wa tatu mfululizo, ratiba ya mwaka huu inavipengele vingi na ilianza kutumika mara tu baada ya kuingia mwezi wa Ramadhani.

Makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya Ustadhat Taghridi Abdul-Khaaliq Tamimi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Quráni, mwezi wa ibada na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kufaidika na utukufu wa mwezi huu Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imeandaa ratiba kamili yenye vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha (maswali na majibu) ambacho ni kipengele cha kielimu chenye maswali mengi ya aina tofauti, maswali kuhusu Quráni, Aqida, Fiqhi na utamaduni, utaratibu wa kuuliza na kujibiwa unasimamiwa na kamati maalum, halafu kamati hiyo huandika maswali na majibu kwenye mtandao rasmi wa mawasiliano ya kijamii ambao upo chini ya idara hii kupitia link ifuatayo: https://www.facebook.com/profile.php?id=100037528393474".

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya pili ni (usomaji wa Quráni) ambao unaratibiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya na kushiriki wanawake peke tu, kila siku saa nne usiku kupitia mtandao wa Telegram, husomwa juzuu moja la Quráni tukufu na hutolewa ufafanuzi wa baadhi ya maneno magumu katika juzuu hilo, halafu washiriki huulizwa maswali kuhusu Quráni, kisha hukusanywa majibu na kusahihishwa na mwisho wa mwezi yatatangazwa majina ya washindi, zawadi za washindi tayali zimesha andaliwa”.

Akasema kuwa: Unaweza kushiriki kwa kuingia kupitia link hii https://t.me/joinchat/AAAAAFjL3MsRhywPJpP3KA.

Akamaliza kwa kusema: “Ratiba yetu inakipengele cha kueleza hukumu za funga kwa kuchagua mambo muhimu katika mlango wa funga na kuweka maelezo hayo kwenye mtandao wa mawasiliano ya kijamii kwa lugha ya kiarabu na kiengereza”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: