Kwa ushiriki wa wanafunzi (300): Idara ya Quráni inaendelea kufundisha Quráni kupitia mtandao

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya wanawake yenye mafungamano na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kuhifadhisha Quráni na kufundisha hukumu za usomaji wa Quráni na kufafanua maana ya baadhi za aya pamoja na kueleza hukumu za kifiqihi.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kuwa: “Kila wiki tunafundisha wanafunzi zaidi ya (300) kutoka ndani na nje ya nchi, tutaendelea kufanya hivyo kwa muda wa mwaka mzima, wanafundishwa kwa kufuata mfumo maalum ulio andaliwa na wasomi bobezi wa Quráni”.

Akaongeza kuwa: “Masomo yanahusu usahihishaji wa usomaji, kwa kuwasikiliza na kuwatahini pamoja na kufanya mashindano”.

Akabainisha kuwa: “Kuna masomo yalikua yanafundishwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, lakini kutokana na tishio la maambukizi ya virusi vya Korona hivi sasa yanafundishwa kwa njia ya mtandao, yanahatua tatu kama ifuatavyo:

Hatua ya kwanza: Mwanafunzi anafundishwa mambo ya awali katika usomaji kwa njia rahisi itakayo muwezesha kuendelea na hatua inayo fuata.

Hatua ya pili: Wanafundishwa hukumu za usomaji wa Quráni, katika hatua hii hupewa mitihani ili kupima uwelewa wao, ukizingatia kuwa wanao uwezo wa kusoma Quráni na kuendesha vikao vya usomaji wa Quráni, huhusisha pia walimu wa masomo ya kiislamu.

Hatua ya tatu: Nayo ni muhimu sana, walengwa wa hatua hiyo ni wanafunzi wenye umri wa miaka (16 hadi 30), hufundishwa hukumu za usomaji wa Quráni, kuhifadhi Quráni na tafsiri, pamoja na kufanya mitihani ya mara kwa mara ili kuimarisha uwelewa wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: