Kamati ya maelekezo na misaada imegawa chakula cha Ramadhani kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na taasisi ya Answaaru-Zaharaa (a.s) Alkhairiyya, wamegawa chakula kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.

Walianza kazi ya kugawa chakula tangu ilipotolewa amri ya marufuku ya kutembea, ili kuzisaidia familia zinazo dhurika na marufuku hiyo, ugawaji wa chakula umekuwa ukifanywa chini ya program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) iliyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, kupitia program hiyo zimefikiwa familia nyingi za mafakiri katikati ya mkoa wa Karbala na pembezoni mwake.

Kiongozi wa kamati hiyo Shekh Haidari Aaridhi ameuwambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani huwa tunasaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, lakini mwezi huu imekuwa tofauti, familia zimeongezewa matatizo zaidi baada ya marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, hivyo tunafanya kila tuwezalo kupunguza shida walizo nazo, na kusimama pamoja nao wakati huu wa matatizo”.

Akaongeza kuwa: “Tangu ilipo ingia Ramadhani tumekuwa tukigawa chakula kulingana na mahitaji ya kila mtaa, kwa kushirikiana na wawakilishi wa Marjaa Dini mkuu kwenye mitaa hiyo, mitaa tuliyo ifikia ni: (Mtaa wa Huru, Mtaa wa Askariy, Mtaa wa Yarmuuk, Mtaa wa Jawaad, Mji wa Aamiriyya/ barabara ya Towareji, mji wa Kuraitu/ barabara ya Najafu, Mtaa wa Muhandisina na Mtaa wa Alghadiir), bado tunaendelea kugawa chakula chini ya ratiba maalumu iliyo pangwa”.

Kumbuka kuwa chakula wanacho gawa ni mjumuiko wa aina mbalimbali ambazo ni muhimu kwa familia hizo, imechaguliwa mitaa ya wakazi wa mji wa Karbala na pembezoni mwake kulingana na hali ya maisha ya watu wa mitaa hiyo, na imepewa kipaombele zaidi mitaa ambayo asilimia kubwa ya wakazi wake wanapata riziki zao kwa kufanya kazi za kila siku, kama alivyo himiza Marjaa Dini mkuu ulazima wa kuunganisha nguvu na kusaidia mafakiri na watu wenye kipato kidogo kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ndio Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ambao ndio waathirika wakubwa na marufuku ya kutembea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: