Kwa kutumia vifaa kwa kisasa: Wakati wa jioni kazi ya kupuliza dawa inaendelea katika mitaa ya mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kamati iliyo undwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) inaendelea kupuliza dawa katika mitaa ya mkoa mtukufu wa Karbala, katika mkakati wake wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, jana wamepuliza katika mji wa Imamu Hussein (a.s) na mtaa wa Usra na Mulhaqu, kwa kutumia vifaa vya kisasa walivyopata hivi karibuni kwa ajili ya kazi hiyo.

Mjumbe wa kamati hiyo Ustadh Abbasi Hassan Abdu-Ali amesema kuwa: “Tumetumia zaidi ya lita elfu sita za dawa chini ya usimamizi wa jopo la madaktari na wataalamu, kazi hii ni muendelezo wa kazi zingine zilizo fanywa na Ataba kwa zaidi ya siku 45 hapa katika mji wa Karbala, tumesha puliza katika mitaa, miji, taasisi za serikali, barabara, viwanja na kila mahala, bado tunaendelea kuwatumikia wananchi wetu watukufu”.

Kumbuka kuwa kazi hii ilianza kufanywa siku nyingi, kasi ikaongezeka zaidi baada ya Marjaa Dini mkuu kuhimiza ulazima wa kusaidia sekta ya afya katika mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: