Idara ya shule za wasichana Alkafeel imetangaza matokeo ya hatua ya pili ya shindano la (njia ya uokovu)

Maoni katika picha
Idara ya shule za wasichana Alkafeel imetangaza matokeo ya hatua ya pili ya shindano la (njia ya uokovu) yaliyo husisha wanawake peke yake, yaliyo kuwa na maswali ya Fiqhi, Aqida na masomo mengine.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika shindano hili lililodumu kwa muda wa siku tano tumepata zaidi ya washiriki (700), majibu sahihi yaliyo pigiwa kura yalikuwa (180), majibu (50) kutoka kwa washiriki hamsini wameshinda”.

Akaongeza kuwa: “Katikati ya mwezi huu tutafanya shindano lingine ambalo tumelipa jina la (Rauhu wa Raihanu), litakalo husisha mabinti wenye umri wa miaka (6) hadi (12) katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan (a.s)”.

Kumbuka kuwa idara ya shule za wasichana Alkafeel chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani tangu siku ya kwanza ya mwezi huu, ratiba hiyo inavipengele vifuatavyo:

  • - App ya (Haqiibatu-Swaaimu) nayo ni program maalum inayofanya kazi kupitia simu ganja (smartphone) ambayo imejaa muongozo wa ibada za mwezi wa ramadhani.
  • - Hatua ya pili ya shindano la (njia ya uokovu) lenye maswali ya Fiqhi, Aqida na masomo mengine.
  • - Shindano la (Qutufu-Ramadhaniyya) nalo linaendelea mwezi mzima wa Ramadhani na linarushwa kupitia chanel ya Istighaathah.
  • - Shindano la (Rauhu wa Raihanu) litakalo husisha mabinti wenye umri wa miaka (6) hadi (12) katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan (a.s).
  • - Hatua ya tatu ya shindano la (njia ya uokovu) litaanza katikati ya mwezi mtukufu wa Ramadhani pia.

Tambua kuwa ratiba hii inalenga kujenga uwelewa wa Dini kwa wasichana wa kiislamu, na kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani katika kuongeza maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: