Mwezi kumi na mbili Ramadhani: Ni siku ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu uliunga undugu kati ya Muhajirina na Answaru na yeye na ndugu yake mtoto wa Ammi yake Ali

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi kumi na mbili Ramadhani, Mtume (s.a.w.w) aliunga undugu kati yake na kiongozi wa waumini Ali (a.s) baada ya kufanya hivyo kati ya Muhajirina na Answaru.

Kazi ya kwanza aliyofanya Mtume (s.a.w.w) baada ya kujenga msikiti ilikuwa ni kuunga undugu, amboa ndio kiunganishi kikuu baina ya Muhajirina na Answaru, chenye mizizi ya Imani na msindi wa upendo, kusaidiana, kulindana, pamoja na usawa katika mali, jambo kubwa lililo waunganisha lilikuwa ni kuunga undugu, aliwahi kuunga undugu baina ya Muhajirina kwa ajili ya kutendeana haki na usawa wakiwa Maka kabla ya kuhama, na baada ya kuhama Maka akaunga undugu kati ya Muhajirina na Answaru katika mji wa Madina.

Imepokewa katika riwaya kuwa, pindi Mtume (s.a.w.w) alipo unga undugu baina ya maswahaba wake, Ali (a.s) alimfuata akiwa macho yake yanalengalenga (mwenye huzuni), akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu umeunga undugu baina ya maswahaba wako na mimi hujaniunga ungugu na yeyote?! Mtume (s.a.w.w) akamuambia: Wewe ni ndugu yangu duniani na akhera.

Abu Tamami anasema:

Ni ndugu yake wa pekee na mkwe wake * hakuna ndugu wa mfano wake wala mkwe kama yeye.

Jambo la kuunga undugu lililofanywa na Mtume (s.a.w.w) ni siasa kubwa ya kiislamu iliyo himizwa na Quráni tukufu, Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Hakika waumini ni ndugu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: