Mashindano ya Quráni ya kitaifa yanaendelea kwa njia ya masafa na yameingia hatua ya pili

Maoni katika picha
Hatua ya kwanza ya mashindano ya Quráni ya kitaifa yanayo simamiwa na Maahadi ya Quráni awamu ya kwanza kwa vikundi nane kupata alama za juu katika jumla ya vikundi (21) vilivyo shiriki kutoka mikoa tofauti ya Iraq.

Vikundi vinavyo jiandaa kuingia hatua ya pili ni: (kikundi cha Najafu, kikundi cha Misaan, kikundi cha Mubswiriin, kikundi cha Baabil, kikundi cha Muthanna, kikundi cha Bagdad/A, kikundi cha Karbala na kikundi cha Bagdag/B).

Awamu ya pili ya mashindano itakuwa ya mtowano, kila kundi zitashinda tim mbili ambazo zitaingia kwenye hatua ya tatu ya mashindano haya.

Tambua kuwa mashindano ya Quráni ya kitaifa yanayo simamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika kila mwezi wa Ramadhani yanafanywa kwa mara ya sita mfululizo, kwa ushiriki wa vikundi (21) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, mara hii yanafanywa kupitia njia ya mtandao, kutokana na kuheshimu maelekezo ya idara ya afya kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa mashindano haya yanahusisha sauti, naghma, tafsiri na kaswida pamoja na maswali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: