Hospitali ya rufaa Alkafeel inatibu marhadhi ya ngozi kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa

Maoni katika picha
Kituo cha maradhi ya ngozi katika hospitali ya rufaa Alkafeel inamiliki vifaa viba vya kisasa vinavyo tibu kila aina ya maradhi ya ngozi.

Bingwa wa magonjwa ya ngozi katika hospitali ya Alkafeel Dokta Swadiq Jafari amesema: “Hakika kituo cha maradhi ya ngozi katika hospitali ya Alkafeel kinavifaa tiba vya kisasa, kikiwemo kifaa cha (EXCIMER) na kifaa cha (UV) na vifaa vya kutumia mionzi, na vinginevyo miongoni mwa vifaa tiba vya kisasa vyenye uwezo wa kutibu aina zote za maradhi ya ngozi”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kinapokea aina zote za maradhi ya ngozi kama vile, upele, baranga, mkanda wa jeshi, nk..”.

Akafafanua kuwa: “Hali kadhalika kinapokea watu wenye maradhi ya kupasuka ngozi, matatizo ya kucha, nywele, mashilingi ya kichwani, maradhi ya viganja vya mikono, kuchubuka ngozi, kwa ufupi kila aina ya maradhi ya ngozi yanatibiwa kwenye kituo hicho”.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel kila baada ya muda fulani hualika madaktari bingwa wa maradhi ya aina mbalimbali, sambamba na kupokea wagonjwa wa kila aina ambao wapo katika kila hali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: