Namna gani lilianzishwa kongamano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s)?

Maoni katika picha
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) Sayyid Aqiil Abdulhussein Yaasiriy amesema kuwa, watu wa mji wa Hilla ndio waanzilishi wa kongamano hili, walianza wakati wa serikali ya kidikteta iliyo pita na utambulisho wa mji wao ukawa: (Hilla ya Imamu Hassan Mkarimu wa Ahlulbait –a.s-) jina la mji wao likaunganishwa na jina tukufu la Imamu.

Akaongeza kuwa: “Jina hilo (Hilla ya Imamu Hassan –a.s-) lilianza kutumika katika miaka ya stini karne iliyo pita, Mheshimiwa Sayyid Muhsin Hakim alipo shauri kila mkoa wa Iraq ufungamanishwe na jina la Imamu Maasumu, kama sehemu ya kulipa utukufu jina lake la asili”.

Akabainisha kuwa: “Watu wa mji wa Hilla walianza kufanya kongamano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kila mwaka, wakafanya miaka mitatu mfululizo halafu wakashindwa kuendelea kwa sababu ya mateso waliyo kuwa wanafanyiwa na uongozi wa kidikteta ulio pita, sambamba na kushambuliwa fikra na madhehebu ya Ahlulbait (a.s), wakarudi tena kufanya kongamano hilo baada ya kuanguka utawala huo mwaka (2003) chini ya usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kongamano hilo lina vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni: (vikao vya kuwasilisha mada za kitafiti, shindano la kuandika kitabu kuhusu Imamu Hassan –a.s-, vikao vya usomaji wa Quráni na mashairi, maonyesho ya vitabu na fani zingine za sanaa”.

Akafafanua kuwa: “Lengo la kufanya kongamano hili ni kuonyesha nafasi ya Imamu (a.s) na namna alivyo pambana na utawala wa Muawiya, sambamba na kuangalia changamoto na mitihani aliyo pata katika maisha yake, pamoja na kuipatia dunia vitabu vinavyo mzungumzia bila kusahau baadhi ya wasia wake na hadithi za Imamu katika mambo ya tabia njema na falsafa ya ibada”.

Akasisitiza kuwa: “Awamu ya kumi na tatu haijafanywa kama ilivyo zoweleka, imefanywa kutipia mitandao ya mawasiliano ya kijamii, pamoja na kutoa zawadi kwa madaktari na askari wa mji wa Hilla”.

Kumbuka kuwa kongamano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) husimamiwa na watu wa mji wa Hilla (Mji wa Imamu Hassan –a.s-) chini ya ufadhili wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kila mwaka hufanywa katika mji wa Hilla, makao makuu ya mkoa wa Baabil/ Maqaam Radu-Shamsi, katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wa kwanza wa Mtume Muhammad Imamu Hassan mtoto wa Ali (a.s) ambaye alizaliwa mwezi kumi na tano Ramadhani, kongamano hilo hufanywa mwezi (14 – 16) Ramadhani kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: