Shamba boy wa chuo kikuu cha Alkafeel wameweza kujitosheleza katika miti ya mauwa

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kimetangaza kuwa wamejitosheleza katika sekta ya miti ya mauwa kwa mahitaji yote ya chuo, na katika kila msimu kulingana na mahitaji ya bustani zake.

Makamo rais wa chuo katika mambo ya utawala Dokta Farasi Usfuur amesema kuwa: “Hakika chuo kikuu cha Alkafeel kina utaratibu kinaofuata, miongoni mwa vipengele muhimu katika utaratibu huo ni kuhakikisha kuwa inajitegemea katika kazi zake, vitalu vya chuo ni moja ya sehemu za kujitegemea, wamefanikiwa kujitosheleza katika miti na mauwa pamoja na kuwa na muda mfupi tangu kuanzishwa kwake”.

Akaongeza kuwa: “Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mauwa na miti ya kivuli sambamba na kuweka mazingira vizuri ya bustani, idara ya kilimo katika chuo chetu imeanzisha vitalu maalum, vitakavyo wezesha kukidhi mahitaji yake na zaidi itauzwa kwa bei nafuu”.

Mhandisi Ali Aamiriy kiongozi wa idara ya kilimo katika chuo hicho amesema kuwa: “Mradi huu ulianza kwa kupanda aina tano za mauwa na miti ya msimu na isiyokuwa ya msimu, pamoja na miche mingine ya aina mbalimbali, kwa hakika tumeweza kupanda mauwa na miti ya mapambo katika bustani zetu kutokana na miche tuliyo andaa sisi wenyewe, kisha tataanza kuandaa miche ya kupanda mashambani kwa ajili ya kilimo”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kimeweka umuhimu mkubwa katika kuboresha vitalu vyake kwa kupanda miche ya mauwa na miti tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: