Kikosi cha Abbasi kinaendesha opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika mkoa wa Basra

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za kupamnana na maambukizi ya virusi vya Korona, watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wanaendesha opresheni kubwa ya kupuliza dawa kwenye mitaa ya mkoa wa Basra.

Kiongozi anaye wakilisha kikosi Ustadh Amiin Twaaiy amesema kuwa: “Kazi hii inafanywa kwa kushirikiana na kituo cha jeshi la wananchi cha mkoa wa Basra, imehusisha kitongoji cha Ahraar na mtaa wa Asaatidhah (barabara nne)”.

Akaongeza kuwa: “Tumetumia vifaa vya kisasa pamoja na gari nne ambazo kila moja ilikuwa na tenki lenye tani moja ya dawa na watu kumi na moja wenye tenki za kubeba mgongoni ambao wanapuliza dawa kwa mikono”.

Akasema: “Tutaendelea na kazi hii katikati ya mji wa Basra chini ya maelekezo ya idara ya afya ya mkoa huo, hususan katika kubaini maeneo yanayo hitaji kupuliziwa dawa”.

Kazi hii inatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata muongozo wa idara ya afya katika shughuli za kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimesha fanya opresheni nyingi za kupuliza dawa kwenye miji tofauti na bado kinaendelea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: