Mwezi wa Ramadhani katika kumbukumbu ya Karbala: usiku wa Lailatul-Qadri na uhuishwaji wake

Maoni katika picha
Karbala ni mlango miongoni mwa milango ya Mwenyezi Mungu katika ardhi yake, yawezekana ukawa ni mkubwa na uliokaribu yake zaidi, kwa sababu moyo wa kufanya toba na kuomba maghafira umeota mizizi kuanzia yalipotokea mauwaji wa Twafu nuru ya Mwenyezi Mungu ikaangaza katika ardhi ya Karbala kwa kuuwawa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).

Baada ya hayo niliyo sema unaweza kufikiri usiku ambao Quráni ilitelemshwa utakuwa namna gani katika mji unao angaziwa na nuru ya Mwenyezi Mungu kwa mamia ya miaka?! Unaweza kujuwa usiku huo unanafasi gani katika nafsi za watu wa Karbala?!

Mmoja wa wakazi wa Karbala anaeleza kuhusu usiku huo kwenye miaka ya sitini na sabini, naye ni Ustadh Ali Khabaaz kiongozi wa idara ya habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu: “Miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakifanywa na watu wa Karbala katika usiku wa Lailatul-Qadri ni kukesha wakifanya ibada ndani ya haram takatifu (Nakusudia uwanja wa haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi –a.s-) husomwa dua za usiku wa Lailatul-Qadri ikiwemo ile ya kuweka msahafu kichwani, walikuwa watu wote wa Karbala wanashiriki kwenye ibada hizo, tunacho shuhudia hivi sasa usomaji wa dua na majlisi za Husseiniyya ni urithi kutoka kwa wazee wetu kwa mamia ya miaka, ufanyaji wa ibada katika usiku wa Lailatul-Qadri hauishii ndani ya haram mbili peke yake, bali hufanywa katika misikiti na husseiniyya na kila mahala”.

Akaongeza kuwa: “Kuna jambo lingine pia ambalo watu wa Karbala wamezowea kulifanya katika usiku wa Lailatul-Qadri wa mwezi 23 Ramadhani, utawakuta kila mmoja anashauku ya kufuturisha wenzake, jambo hilo huanza mwanzoni mwa mwezi, na huzidi katika usiku wa Lailatul-Qadri, utawakuta wanaandaa futari na kuigawa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: