Mihadhara ya mwezi wa Ramadhani inatolewa kila siku ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu inavipengele vingi vinavyo tekelezwa kwa kufuata maagizo na maelekezo yaliyo tolewa na wizara ya afya kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, miongoni mwa vipengele hivyo ni utowaji wa mihadhara ya kila siku chini ya uhadhiri wa Shekh Swahibu Twaaiy ndani ya ukumbi wa utawala na kurushwa na mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Kwa mujibu wa maelezo ya Shekh Twaaiy kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema: “Mihadhara hii ni muendelezo wa majlisi kubwa zilizokuwa zinafanyika ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku baada ya swala ya Magharibaini, zilikuwa zinahudhuriwa na watu wengi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, lakini kutokana na mazingira ya sasa, ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na maelekezo ya wizara ya afya kuhusu jambo hilo, pamoja na muongozo wa Marjaa Dini mkuu wa kujiepusha na misongamano kwa ajili ya kuepuka uwezekano wa kutokea kwa maambukizi, mwaka huu tumetosheka na kufanya majlisi ya watu wachache ndani ya ukumbi wa utawala, na kurushwa kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii pamoja na baadhi ya vituo vya luninga, baada ya kuandaliwa na kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Twaaiy akaongeza kuwa: “Mihadhara inatolewa kwa kufuata ratiba maalum, kuna mada za malezi, Aqida, Akhlaqi pamoja na mada za kumjenga mwanaadamu na jamii katika kupambana na changamoto mbalimbali, ikiwemo ni pamoja na mambo yanayohusu janga la Korona, aidha huongelewa pia matukio ya kidini yaliyopo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kama vile kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), kifo cha Abu Twalib na bibi Khadija (a.s) pamoja na kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s)”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalum inayo tekelezwa mchana na usimu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufuata tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: