Kiongozi wa idara Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kuwa: “Hakika App ya (Iqraa wa arq) inahusu usomaji wa Quráni kila siku, inawasomaji (150) nayo ni App ya aina ya pekee”.
Akafafanua kuwa: “Wazo la kuanzishwa kwa App hii limetokana na kutaka kudumisha usomaji wa Quráni wa kila siku ndani ya kipindi chote cha mwaka mzima, na wala sio katika mwezi wa Ramadhani peke yake, kwa kuweka ratiba maalum ya kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu kila siku”.
Akabainisha kuwa: “Wanaweza kushiriki kwenye kisomo hicho wanaume na wanawake kutoka kila sehemu ya dunia, thawabu za kila kisomo zikaelekezwa kwa mmoja wa maasumina (a.s), App inamambo yafuatayo:
- - Masomo ya Fiqhi, Tafsiri na malezi, msomaji anaweza kufuata usomaji sahihi.
- - Mshiriki atafahamishwa utukufu anaopata duniani na akhera.
- - Kuna wasomaji mia moja na hasini wanao soma kila siku ndani ya miezi mitano, nao huanza baada ya kurekodi wasomaji.
- - Inatoa nafasi ya kushiriki katika ziara kwaniaba.
- - Unaweza kushiriki usomaji wa pili katika wakati muwafaka kwako”.
Akasisitiza kuwa: “Kushiriki usomaji wa Quráni kila siku, kutakufanya ufuatilie usomaji wa kwenye App jabo kwa robo hizbu ndani ya miezi (5) na utaweza kumaliza Quráni”.