Kitengo cha malezi na elimu ya juu kimefanya mkutano na idara ya shule za Al-Ameed kujadili namna ya kufanya mitihani

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kufanyia kazi maamuzi yaliyo tolewa na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, kuhusu mitihani ya wanafunzi wa darasa la kwanza ya (nusu mwaka) kwa masomo ya mwaka (2019/2020), mheshimiwa mkuu wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Swabihi Kaábiy amefanya kikao na idara ya shule za Al-Ameed, kujadili maandalizi ya mwisho ya mitihani ya masomo ambayo hayakufanyiwa mitihani mwishoni mwa mwezi wa pili uliopita.

Mkutano huo ulikuwa na majadiliano makali kuhusu namna ya kufanya mitihani wakati huu wa kujikinga na maambukizi ya Korona, na kuhakikisha usalama wa wanafunzi na walimu, miongoni mwa mambo muhimu ni kuhakikisha hawasababishi msongamano na kuwapa elimu ya kukaa kwa umbali unaotakiwa.

Dokta Ka’abiy amebainisha kuwa: “Mkutano huu unafanyika wakati muhimu wa kuweka mikakati ya kufanya mitihani kwa kufuata maelekezo ya kikosi cha kupambana na janga la Korona”.

Akabainisha kuwa: “Tumekubaliana na walimu kufanya mitihani katika siku tofauti, kwa ajili ya kujiepusha na msongamano na kutoa nafasi ya kupuliza dawa, walimu na watahaniwa watalazimika kuvaa barakoa kabla ya kuingia eneo la shule, baada ya kumaliza mtihani mwanafunzi ataendelea kukaa kwenye kiti chake hadi mzazi/mlezi atakapo kuja kumchukua na kumpeleka nyumbani ili kusiwe na kuingiliana kati yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: