Malipo ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kutoka kwa Imamu Baaqir kutoka kwa baba yake Sajjaad (a.s) anasema:

Inapoingia siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal muitaji huita, enyi waumini nendeni katika malipo yenu.. kisha akasema: ewe Jaabir malipo ya Mwenyezi Mungu sio kama malipo ya wafalme, halafu akasema: ni siku ya malipo.

Utowaji wa Mola mlezi umeenea kila sehemu, huwarehemu wapenzi wake katika siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na huwalipa waumini walio tenda mema, huwasamehe dhambi waliofunga, ni wajubu wetu sisi waja wake kumshukuru na kupokea malipo, kwa kukamilisha ibada zetu na kufanya ibada kwa wingi katika siku hiyo na kujikurubisha kwake, tusisahau kutakasa nafsi zetu na kufanya wema, tusije tukapoteza ladha ya ibada tulizo fanya mwezi mzima, tusiwe kama baadhi ya watu wanaojali vitu katika siku hii, na wakasahau kufanya jambo muhimu na kuwa sababu ya kupoteza malipo yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: