Idara ya Quráni imetangaza kufanya shindano la (hazina za maarifa)

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake ambalo limefungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya imetangaza shindano liitwalo (hazina za maarifa) kwa njia ya mtandao, washiriki wa shindano hilo ni wanawake tu.

Kiongozi wa idara Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kuwa: “Mwishoni mwa msimu wa Quráni mwezi mtukufu wa Ramadhani, idara ya Quráni imetangaza shindano la (hazina za maarifa), ili nyoyo za waumini ziendelee kunufaika na hazina ya elimu iliyopo katika kitabu cha Mwenyezi Mungu”.

Akafafanua kuwa: “Shindano linamaswali (30), kuna maswali ya irabu, sayansi, tafsiri za baadhi ya aya na hadhithi za Maasumina (a.s) kuhusu baadhi za aya”.

Akasisitiza kuwa: “Mshiriki atasikiliza aya ya Quráni, kisha atajibu maswali atakayo ulizwa, shindano linalenga kujenga utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni kwa wasichana, kwani wao ndio msingi wa malezi ya familia na jamii kwa ujumla, aidha ni sehemu ya kuongeza maarifa katika mambo ya Dini”.

Akaongeza kuwa: “Shindano litadumu kwa muda wa siku nne, mshiriki asiwe na umri wa chini ya miaka (18), majina ya washindi yatatangazwa kwenye mtandao wa Alkafeel, na washindi watapewa zawadi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: