Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mikoa tofauti hapa Iraq

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kupitia wawakilishi wao wa mikoani wanaendelea kupuliza dawa kwenye vijiji na miji tofauti hapa nchini kwa ajili ya kupambana na janga la Korona, wanatumia vifaa vya kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kupambana na kuenea kwa virusi na bakteria.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: baada ya kuongezeka idadi ya maambukizi katika siku za nyuma, viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wakatoa agizo la kupuliza dawa katika miji yote iliyo ripoti visa vya maambukizi, tumepuliza dawa kwenye nyumba za makazi, sehemu za mikusanyiko ya watu na maeneo mengine kwa kushirikiana na idara za afya za maeneo hayo pamoja na jeshi la wananchi.

Akasema: kazi yote imefanywa kwa kutumia vifaa vya kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kupambana na bakteria pamoja na virusi.

Tambua kuwa kazi hii inatokana na wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya, pia ni sehemu ya mkakati wa kikosi cha Abbasi wa kupambana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona hapa nchini.

Kikosi kiliunda jopo maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona mara tu baada ya kupatikana virusi hivyo hapa nchini, jopo hilo limekuwa na jukumu la kupuliza dawa kwenye nyumba za makazi na katika mikusanyiko ya watu hapa Karbala na kwenye mikoa mingine ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: