Katika kusaidia kulinda turathi za mkoa wa Karbala, Atabatu Abbasiyya imeanzisha opresheni ya (Turathi zako ni amana)

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha wa nakalakale na faharasi chini ya maktaba na Daru Mahktutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanzisha program ya (Turathi zako ni amana) inayo saidia kulinda turathi za mkoa mtukufu wa Karbala na kuzienzi upya, kimetoa wito kwa familia za wakazi wa Karbala na Iraq kwa ujumla wa kushiriki katika program hiyo, kwa kutuma turathi au nakalakale za kihistoria kwenye kituo hicho.

Haya yamesemwa na kiongozi wa kituo Ustadh Swalahu Mahadi Siraji: “Malikale ni hazina za kihistoria tulizo achiwa na wazazi wetu zinazo tuonyesha hatua walizo pitia, ni sawa na kauli zao zinazo tuambia mambo yaliyotokea katika zama zao, hivyo huturahisishia kuandika habari za kale kwa kutumia ushahidi wa wazi wa taarifa muhimu zinazo patikana kwenye turathi hizo, ambazo zilikua zimesha anza kutoweka vichwani mwa watu”.

Akabainisha kuwa: “Jambo hili linatokana na umuhimu wa kulinda malikale za Iraq kwa ajili ya historia ya taifa letu, na kuzikusanya upya na kuzihifadhi sehemu maalum baada ya kusambaa, tumeomba ushirikiano kwa familia ambazo zimetunza turathi kutoka kwa mababu zao waje wazikabidhi kwa ajili ya kuzitunza kwenye hazina ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuwafanya kuwa sehemu ya utunzaji wa turathi za taifa lao”.

Akafafanua kuwa: “Tutawapa zawadi watu watakao saidia kufanikiwa kwa program hii, pamoja na kuwapa shukrani maalum kwa mchango wao wa kutunza malikale (turathi), tunatarajia kupata mafanikio katika swala hili la kutoa vumbi kwenye turathi zetu na kuzienzi upya”.

Naye Ustadh Muhammad Baaqir kiongozi wa kitengo cha malikale katika kituo cha upigaji picha wa nakalakale na faharasi amesema kuwa: “Tumechukua jukumu la kuwasiliana na familia zilizo tunza turathi na malikale ili kuzikusanya pamoja na kuziweka katika usalama zaidi, pamoja na kuandika historia ya kila malikale pamoja na familia iliyo itunza na kisha kuikabidhi katika hazina ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kwa ajili ya kutoa taarifa ya turathi au kuwasiliana na kituo, unaweza kutumia toghuti ifuatayo:

  • - https://alkafeel.net/library/photos/
  • - Au ukurasa wa facebook: https://www.facebook.com/mpualkafeel2019/ au Whatsap kwa simu namba: (07700964991).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: