Waziri wa vijana na michezo amesema kuwa: Nilicho kiona katika hospitali ya rufaa Alkafeel kipo sawa na yaliyopo kwenye hospitali za kimataifa

Maoni katika picha
Waziri wa vijana na michezo Sayyad Adnani Darjali amesema kuwa huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel zinalingana na zile zinazo tolewa na hospitali za kimataifa bali zinazidi baadhi ya hospitali hizo, amepongeza huduma za matibabu wanazo pewa wananchi katika hospitali hiyo.

Ameyasema hayo katika ziara yake ya siku ya Jumatano (10 Juni 2020m) baada ya kufika hospitalini hapo akiwa na ujumbe alio fuatana nao, miongoni mwa ujumbe huo ni katibu mkuu wa wizara, mkuu wa mkoa na makamo wake, ugeni huo ulipokelewa na kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya pamoja na mkuu wa hospitali na marais wa vitengo.

Sayyid Darjali akasema: “Tunafuraha kubwa kwa ushirikiano tuliopewa na hospitali ya rufaa Alkafeel ikiwa ni pamoja na kusaini makubaliano rasmi ya ushirikiano hospitali na wizara”.

Akasema: “Tunaona fahari kubwa kuwa na hospitali kama hii hapa Iraq, tuna ushirikiano mzuri kati ya wizara na Ataba tukufu”.

Akamaliza kwa kutuma salam na shukrani nyingi kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na viongozi wote wa Ataba, kutokana na huduma kubwa wanazo towa kwa raia wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: